OXFARM YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KIBONDO


Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Dr. Pima Sebastian akipokea msaada wa vifaa vya kupambana na Corona na maafa mengine yanayoweza kujitokeza kutoka kwa Mratibu wa Miradi ya Oxfarm Kanda ya Ziwa Bw. Valentine Shipula.

Shirika la oxfarm kupita mradi wa kupunguza athali za maafa limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 29 katika hospitali ya Wilaya ya Kibondo ili kupambana na janga la corona na maafa mengine yanayoweza kujitokeza. 

Akizungumza na blog hii mda mfupi baada ya kutoa vifaa hivyo mratibu wa miradi ya oxfarm kanda ya ziwa Bw. Valentine Shipula amesema kuwa miongoni mwa vifaa hivyo ni pamoja na barakoa  970 za chumba cha upasuaji, mavazi 58 yanayovaliwa katika chumba cha upasuaji na barakoa za kawaida pakti 240. 

Aidha amesema kuwa kupitia mradi wa kupunguza athali za maafa shirika la oxfarm limeamua kutoa misaada hiyo katika Wilaya za Kibondo, Kishapu pamoja na Msalala ili kusaidia kupunguza athali za ugonjwa wa corona ambazo zingeweza kutokea. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Dr. Pima Sebastian akipokea msaada huo amesema kuwa mwenendo wa ugonjwa wa corona umepungua lakini vifaa hivyo vitasaidia hata katika magonjwa mengine ya mlipuko ambayo yanaweza kutokea.

Post a Comment

0 Comments