WATOTO WAWILI WAFARIKI NA MMOJA ANUSURIKA, MAMA YAO AKISHIKIRIWA POLISI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Filimon Makungu


Na Mwajabu  Kigaza, Kigoma.

WATOTO wawili wenye umri chini ya miaka mitano wamefariki dunia na mwingine mwenye umri wa miaka saba akinusurika kifo kwa madai ya kulishwa sumu na mama yao mzazi aliyefahamika kwa jina la Christina Akoonay  kisha na yeye kunywa sumu katika Mtaa wa Shede Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.

Akielezea tukio hilo kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Filimon Makungu amesema tukio hilo limetokea Novemba 22 mwaka huu majira ya saa tatu usiku ambapo mama huyo alikutwa ndani ya nyumba wakiwa hawajitambui na motto mmoja aliyejulikana kwa jina la Daniel Deogratius miaka mitano mwanafunzi wa shule ya msingi Calmel akiwa amefariki dunia.

Kamanda Makungu amesema mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya Rufaa Maweni wakiwa wanapatiwa matibabu motto mwingine David Deogratius mwenye umri wa miezi 11 naye alifariki dunia.

Kamanda amewataja Christina Akoonay miaka 36 na Davina Deogratius  miaka saba wakiendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa maweni Mkoani Kigoma na hali zao zikiendelea vizuri huku akieleza jeshi hilo kuendelea kumshikilia mama wa watoto hao kwa uchunguzi zaidi.

Mganga mfawidhi wa Hospital ya rufaa Maweni Mkoani Kigoma Dkt Stanley Binagi amethibitisha kupokea marehemu mmoja, na wengine wakiwa bado hai na kusema kuwa Watoto hao wanasadikiwa kupewa sumu.

“ Tuliwahi kuwapatia huduma walikuwa na hali mbaya sana lakini watoto wawili walifariki dunia kati yao mmoja alipoteza maisha akiwa tayari anapatiwa huduma na hadi sasa hali ya mama inaendelea vizuri japo bado hajaweza kuzungumza vizuri lakini pia kiumbe kilichopo tumboni hakikuadhiriwa na sumu hiyo” alisema Daktari.

Kwa sasa mkoani Kigoma matukio ya ukatali wa kusababisha vifo au kujiua yameonekana kuongezeka kwa kasi ambapo Petro Bwanji kutoka Idara ya Ustawi wa Jamii imeeleza jitihada zake katika kukabiliana changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kuwatumia maafisa ustawi wa jamii kuendelea kutoa elimu kwa jamii.

Baadhi ya Majirani wameeleza kwa siku za karibu walikuwa wakiona familia ikiwa katika hali ya kawaida lakini wameshangazwa na tukio hilo ambapo wamesema kitendo alichokifanya mama huyo ni kitendo kibaya ambacho hata imani za dini zinakataza kitendo kama hicho.

 

 

 


Post a Comment

0 Comments