TARURA YAONGEZEWA BAJETI YA DHARURA.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amsema Serikali imeongeza Bajeti ya dharura ya TARURA kutoka bilioni 21 mpaka bilioni 131, na Bilion 350 zimeogezwa maalumu kwaajili ya ukarabati wa Barabara.

Mhe. Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe. Issa Mtemvu aliyetaka kujua Je Serikali ipo tayari kupeleka fedha maalumu katika Barabara ya Maramba Mawili, King`azi iliyoharibika kutokona na mvua kwaajili ya utatuzi?

  “Serikali inatambua changamoto za kimiundombinu katika maeneo mbali mbali nchini kutokana na mabadiliko ya hali ya tabia ya Nchi na mvua nyingi zinazoendelea, Serikali imetenga fedha ya dharua na kuongeza Bajeti ya TARURA ili kuwezesha ukarabati wa Barabara hizo” Mhe. Katimba.

Pia Mhe. Katimba amesema Serikali inatambua umhimu mkubwa sana wa barabara katika kuwawezesha Wananchi kiuchumi na kijamii hivyo serikali itaendelea kutoa fedha na kuhakikisha barabara zinajengwa ili kurahisisha huduma hizo kote Nchini.

Post a Comment

0 Comments