WAFUGAJI KUKU KIGOMA WADHAMILIA KUFANYA UFUGAJI WENYE TIJA






Diana Rubanguka, Kigoma 
Wafugaji wa Kuku mkoani Kigoma wamesema kuwa wanadhamilia kufanya ufugaji wa tija kwa kuwa ufugaji ni miongoni mwa Biashara ambayo inaweza kumuinua kila mtu atakayekuwa tayari kufuga kwa kufuata utalaamu.

Hayo yameelezwa  Gudila Temba mfugaji wa kuku kutoka Mkoa wa Kigoma wakati wa mafunzo ya kilimo na ufugaji yaliyotolewa na kampuni ya silverlands yenye makao yake makuu mkoa wa Iringa  yaliyofanyika kwa wafugaji wa mkoa wa Kigoma.

Temba amesema, anadhamilia kufuga kwa tija kwa kuwa ameona manufaa aliyoyapata kutokana na kazi hiyo ambapo awali alianza na kuku 100 na sasa unafunga kuku zaidi ya 2000.

"Natarajia kufanya ufugaji wa tija zaidi, nimegundua ufugaji ni biashara mimi binafsi nilianza na kuku 100 tena kwa kuwanunua kwa mfugaji mwenzangu, lakini kupitia hao kuku nimefikia kuku zaidi ya 2000 na sasa naendelea kukua" amesema Temba.

Meneja Mauzo kutoka kampuni ya Silvalands inayojihusisha na kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku Jaremiah Kilato amesema, pamoja na mkakati wa kuzunguka Tanzania nzima kuhamasisha ufugaji wa kisasa wenye tija na wa kibiashara Kigoma imepewa kipaumbele kutokana na mwamko mkubwa ambapo wafugaji wa mkoa huo wameamua kufanya uwekezaji mkubwa kama ilivyo kwa biashara nyingine.

Kutoka na mwamko huo uhitaji wa bidhaa za kampuni hiyo umekuwa mkubwa hivyo kampuni imeamua kuweka uwakilishi wa moja kwa moja ambapo kuna mawakala ambao wanasaidia kuuza bidhaa hizo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wafugaji.

"kipekee Kigoma ulipendekezwa kutokana na mwamko mkubwa ambapo ukifanya uwiano wa ufugaji kwa mwaka jana utofauti ni mkubwa, pamoja na mwamko huo awali kulikuwa na  changamoto ya upatikanaji wa bidhaa zinazosababishwa na sababu za kijiografia zilizopelekea vifaranga kufa na vyakula kulowa Silva lands ikaona ni vyema kuunga mkono juhudi hizo" amesema Kilato.

Hata hivyo Silvalands imeona ni vyema kutoa mafunzo kwa wafugaji ikiwa ni sehemu ya kazi zao na ni mafunzo ambayo mfugaji wa kuku anatakiwa ayapate, ili kuboresha ufugaji wa kuku aina ya kuku nyama, kuku mayai na chotara.

Mafunzo hayo ni pamoja na sehemu ya  usimamizi wa miradi, ulishaji kuku, utoaji chanjo na utunzaji wa kumbukumbu ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kupata uelewa wa kuwakinga kuku na magonjwa ambayo imekua changamoto inayosababisha wafugaji kukata tamaa na wakati mwingine kuua mitaji yao.

Akizungimzia masuala la ya chanjo Happy Tendega kutoka kampuni ya CEVA amesema kuwa, kuku anapaswa kuchanjwa akiwa kifaranga ili kuepuka magonjwa yote wanayomkabiri, ambapo miangoni wa chanjo ni kideri na mafua.

Post a Comment

0 Comments