WAKULIMA WILAYANI UVINZA WAKABILIWA NA NJAA BAADA YA MAZAO YAO KUHARIBIWA NA MVUA



WAKULIMA wa mazao mbalimbali  yakiwemo zao la mpungu na mahindi katika kijiji cha Mpeta, Halmashauri ya Wilaya Uvinza, mkoani Kigoma wamesema wanakabiliwa na njaa baada ya  mazao yao kuharibika kutokana na mvua zilizonyesha mwaka huu.

Wakizungumza na blog hii, wakulima hao akiwemo Bw. Lusendamila Mashaka, walisema mvua za mwaka huu zimekuwa nyingi jambo lililofanya mazao yao kuharibiwa na maji huku kukiwa hakuna chakula kingine watakachotumia.

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji hicho Bw. Juma Ally Kisila, alisema baadhi ya wakulima waliokuwa wamewekeza kwenye zao la mpunga wamepata hasara na hivyo  hawana budi kujenga tabia ya kufuatilia maelekezo ya wataalamu wa hali ya hewa kabla ya kuanza kulima.

Nae Mkuu wa Wilaya hiyo, Bi. Mwanamvua Mlindoko,  amekiri kutokea kwa uharibifu huo huku akisema serikali ya wilaya hiyo imechukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanaepuka kurudi katika maeneo yaliyoathiliwa na mvua.

 


Post a Comment

0 Comments