WANANCHI WA KIJIJI CHA KUMWABU WILAYANI KIBONDO WAJENGEWA KISIMA ILI KUTATUA KERO YA MAJI

Kisima cha maji kilichojengwa kwaajili ya wananchi wa kijiji cha Kumwambu wilayani Kibondo mkoani Kigoma. (Picha Na James Jovin

KAMPUNI ya ujenzi inayotekeleza mradi wa barabara kwa kiwango cha lami katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma SINOHYDRO Corporation Limited imewajengea kisima cha maji wananchi wa kijiji cha Kumwambu kilichoghalimu shilingi milioni 26.5. 

Kisima hicho kimejengwa ili kuwasaidia wananchi wanaozunguka eneo ambalo kampuni hiyo imejenga kituo chake cha kazi ikiwa ni sehemu ya kusaidia jamii inayowazunguka. 

Tatizo la maji katika eneo la kumwambu sasa limepatiwa ufumbuzi kwani wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakipewa huduma ya maji kwa zaidi ya masaa nane kila siku hivyo kuokoa mda wa kufanya shughuli zingine. 

Baadhi ya  wananchi wa kijiji cha Kumwambu wilayani Kibondo mkoani Kigoma wakichota maji katika kisima walichojengewa na kampuni ya SINOHYDRO. (Picha Na James Jovin)

Baadhi ya wananchi waliokutwa wakichota maji katika eneo hilo waliishukuru kampuni ya SINOHYDRO Corporation Limited kwa msaada huo kwa kuwa awali walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma ya maji hivyo kutumia mda mwingi ambao wangefanya shughuli nyingine za kimaendeleo. 


Katika hatua nyingine kampuni ya SINOHYDRO Corporation Limited iko katika hatua za mwisho kuanza ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 25.9 katika wilaya ya kibondo mkoani Kigoma. 

Post a Comment

0 Comments