WATU 9 WAMEFARIKI NA WENGINE 51 KUNUSURIKA BAADA YA BOTI KUZAMA KATIKA ZIWA TANGANYIKA


WATU tisa wamefariki  baada ya boti la abiria kuzama  katika ziwa Tanganyika.

 

Akizungumza na blog hii kwa njia ya simu Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi Martin  Ottieno amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la rasini.

 

Amesema kuwa Boti hiyo  iitwalo Mv Nzeimana linalofanya safari zake kati ya Kijiji cha Sibwesa na Ikola  limezama  likiwa abiria sitini ambapo abiria hamsini na moja wameokolewa.

 

“Watu tisa waliofariki miili yao imeshaopolewa kutoka  majini ambapo kati yao wanawake ni saba na waume wawili, lakini watu 51 wameokolewa wakiwa hai” alisema Kamanda Ottieno

 

Aidha Kamanda Ottieno  amesema chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali uliosababisha boti hilo kukosa muelekeo na hatimaye kupinduka

 

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sibwesa wamesema kuwa kuna baadhi ya miili ya watu ilisukumwa na upepepo mpaka nchi kavu huku wakisema


“Kulingana na hali hiyo kwasasa baadhi ya wananchi wa Sibwesa wamekaa vikundi vikundi kutokana na kupoteza jamaa zao kupoteza uhai”


Nao baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwemo Josephina Richard na Samweli Costatine wamesema changamoto za usafiri wa majini zimekuwa nyingi kutokana na boti kujaza sana abiria  sambamba na mizigo kuwa mingi.

 

“kwakweli tunaomba boti za mizigo ziwe za mizigo tu na boti za abiria ziwe za abiria tu hapo tunaweza kupunguza ajali za majini lakini pia kuwe na vifaa vya kuwasaidia abiria wakati vyom,bo vinapozama” walisema.



Post a Comment

0 Comments