Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof Joyce Ndalichako akifungua chuo cha ufundi Stadi VETA katika kijiji cha Nyamidaho Wilayani Kasulu mkoani Kigoma. |
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof Joyce Ndalichako akikagua chumba kitakachotumika kwa mafunzo ya ushonaji wa nguo. |
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof Joyce Ndalichako akikagua chumba cha mafunzo ya komputa, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga. |
Chuo cha ufundi Stadi VETA kilichopo kijiji cha Nyamidaho wilayani Kasulu mkoani Kigoma. |
WAZIRI wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof Joyce Ndalichako ameeleza kuwa
serikali imetenga takribani shilingi billion 48 kwaajili ya ujenzi wa
vyuo vya ufundi stadi katika halmshauri ishirini na tisa nchini nzima
lengo likiwa ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na vyuo hivyo kufikia mwaka 2025.
Waziri Ndalichako
alizungumza hayo wakati akizundua chuo cha ufundi stadi VETA katika kijiji cha
Nyamidaho wilayani kasulu Mkoani Kigoma kilichogharimu zaidi ya shilingi
milioni 400 katika ukarabati wake baada ya kujengwa tangu mwaka 2014 chini ya
ufadhili wa shirika la Word Vision.
Aidha Waziri Ndalichako ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2019/20 tayari vyuo kumi katika halmashauri mbalimbali nchini vimekamilika huku jitihada za kuongeza vyuo vingine zikiendelea kufanywa ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
“Tunaendelea na ujenzi
wa vyuo vya ufundi stadi katika halmashauri 29 nchini ambapo serikali imetenga
fedha takribani shilingi milioni 48 kwaajili ya ujenzi huo” alisema Waziri
Ndalichako
Chuo hicho ambacho
kilianza rasmi kuto mafunzo mwezi februari mwaka huu ikiwemo mafunzo ya
umeme,ushonaji na kompyuta kina wanafunzi 62 mpaka sasa lakini inaelezwa
kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa mafunzo ya muda mfupi na wanafunzi
160 kwa mafunzi ya muda mrefu.
Mkuu wa mkoa wa
Kigoma wa Kigoma Brigedia Jenerali
Emmanuel Maganga alisema ni jukuma kwa wananchi wa kijiji cha Nyamidaho na mkoa
wa Kigoma kwa ujumla kuchangamkia fursa hiyo ili kuweza kujiajiri ajira
Chuo cha Ufundi veta
katika kijiji cha Nyamidaho wilayani kasulu kinakuwa ni chuo cha pili cha Veta
kwa mkoa wa Kigoma na kutoa wigo mpana kwa kusomea mafunzo ya ufundi stadi kwa
wakazi wa mkoa huu.
0 Comments