WAZIRI WA FEDHA AAGIZA UJENZI WA JENGO LA TAIFA LA TAKWIMU MKOANI KIGOMA KUKAMILIKA HARAKA



Waziri wa Fedha na mipango ya serikali Mh Phillip Mpango akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua ujenzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya takwimu mkoani Kigoma (Picha Na Emmanuel Michael)


Waziri wa Fedha na mipango ya serikali Mh Phillip Mpango (Mwenye tai nyekundu) akiangalia ramani ya jengo la ofisi ya Taifa ya takwimu mkoani Kigoma litakavyokuwa baada ya kukamilika (Picha Na Emmanuel Michael)



Na Emmanuel Michael, Kigoma

 

WAZIRI wa Fedha na mipango ya serikali Mh Phillip Mpango amemuagiza Mtakwimu mkuu wa Serikali kuakikisha ujezi wa jengo la ofisi ya Taifa ya takwimu mkoani Kigoma linakamilika kabla ya mwaka huu kuisha.

 

Waziri mpango aliyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la  ujenzi wa jengo hilo na kuongeza kuwa jingo hilo likikamilika litaboresha utendaji kazi wa watumishi wa idara kuu ya takwimu na kutoa fursa kwa wananchi kupata takwimu kwaajiri ya matumizi yao na matumizi mengine ya serikali.

 

“Maagizo yangu ni hivi, kabla hujastaafu hili jengo liwe limekamilika na lipendeze, pamoja na kuwa dhamana yangu itaisha Raisi mpya atakapoapa kuendelea na awamu nyingine, nikuahikishie kuwa hii kota ya kwanza fedha za kukamilisha jengo zitatolewa na serikali” alisema Waziri Mpango.

 

Waziri Mpango ameongeza kuwa jengo hilo likikamilika litatoa fursa kwa watumishi wa sekta zingine za fedha kufanya kazi zao katika jengo hilo ambapo hapo awali sekta hizo hazikuwa na ofisi maalumu.

 

Awali Mtakwimu Mkuu wa Serikali Albina Chua alisema kuwa lengo ni kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ifikapo Decemba 30, 2020 huku akiomba fedha zitolewe haraka ili kukamilisha ujezi huo kwa wakati

 

“Muheshimiwa Waziri nikuhakikisheie kuwa bodi ya usimamizi ya ofisi ya taifa ya twakwimu itaisimamia menejimenti kwa ukaribu katika kipindi chote cha utekelezaji wa kazi kukamilika ujenzi wa jengo hilo” alisema Albina.

 

Akizungumza kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Msataafu Emmanuel Mganga, Katibu tawala wa Mkoa huu Rashidi Mchata, aliipongeza serikali ya awamu ya tano  kuamua kumalizia ujezi wa jengo la Ofisi ya takwimu mkoa wa Kigoma ulioanza tangu mwaka 1994.

Post a Comment

0 Comments