IDADI YA VIFO VILIVYOTOKANA NA AJARI YA BOTI YAONGEZEKA KIGOMA

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP James Manyama

IDADI ya vifo vilivyotokana na ajali ya Boti katika Ziwa Tanganyika iliyotokea Julai 30 eneo la Makakara kijiji cha rufuga wilayani Uvinza mkoani Kigoma imeongezekana  kufikia watu 10.

Akithibitisha taarifa hizo kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP James Manyama ameeleza jitihada za uokozi zinaendelea ili kujua ni watu wangapi wamekufa katika ajali hiyo ambayo chanzo chake inaelezwa ni kuzidisha abilia katika boti na hali mbaya ya hewa Ziwani

Awali Kamanda Manyama  alitoa taarifa ya watu sita kufariki kutokana na tukio hilo huku idadi kamili ya abilia waliopanda katika boto hilo ikiwa haijajulikana

Mashuhuda na wakazi wa eneo hilo walielezea tukio hilo ajari hiyo ilitokea  saa nne asubuhi ambapo boti hilo lilikuwa likitokea kijiji cha Sibwesa kuelekea Ikora mkoani Katavi

Hata hivyo Kamanda Manyama alisema kuwa taarifa zaidi juu ya tukio hilo zitaendelea kutolewa ambapo mwezi mmoja uliopita ajali kama hiyo ilitokea katika eneo la kijiji cha Simbwesa ambapo watu tisa walifariki kati ya abiria 60 waliokuwemo katika boti.

 


Post a Comment

0 Comments