Waandishi wa habari za mtandaoni wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kikao cha kutathimini mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binaadam kwa kutumia takwimu(DDA)
Mratibu wa Arusha press club na ofisa mipango wa mradi Seif Mangwangi akizungumza jambo wakati wa kikao cha tathimini ya mradi. |
Na Editha Karlo,Dodoma
WAANDISHI wa habari wa vyombo vya habari mbadala (altenative media) wametakiwa
kufuata maadili ya uandishi ikiwemo kuandika habari za ukweli na za uhakika ili
kuepuka upotoshaji unaoweza kuleta migogoro.
Wakili wa kujitegemea James Marenga aliyasema hayo jana kwenye ukumbi wa
Royal village jijini Dodoma kwenye kikao cha tathmini ya mradi wa utetezi
na ushawishi wa Haki za binaadamu, mradi unaotekelezwa na waandishi wa habari
wa vyombo mbadala nchini kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara na visiwani.
Marenga alisema kuwa waandishi wa habari za mtandaoni wanatakiwa
kuandika habari kwa usawa na ukweli zaidi kwasababu wamekuwa wakiripoti matukio
papo kwa papo ambao hujulikana kama waandishi wa habari za chap chap mtandaoni
hivyo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia maadili ya uandishi.
Pia aliwataka waandishi wa habari kutokuchanganya uandishi wa habari na
siasa, huku akisisitiza kuwa endapo mwandishi wa habari anataka kuwa mwana
siasa basi aachane na kazi ya uandishiwa habari.
"Mwandishi wa habari unajihusisha na siasa kupitia labda chama
chochote unadhani kupitia uandishi wako unaweza kutendea haki vyama vingine
kwenye kazi yako, ukiamua kuwa mwanasiasa kama wewe ni mwandishi wa habari basi
huku inabidi utoke, taaluma ya uandishi wa habari ni tofauti na taaluma
zingine"alisema
Mwenyekiti wa club ya Arusha Press Club Claud Gwandu ambao ndio
wasimamizi wakuu wa mradi huo aliwataka wanahabari kufuata sheria zilizopo hata
kama hawakubalina na sheria hizo wakati asasi zao zikiendelea kuwasiliana na
serikali kuona namna bora ya kurekebisha sheria hizo.
Naye Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo mbadala (Altenartive
media) Midraji Ibrahimu aliwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili ya
uandishi wa habari hususanu katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye kampeni na
uchaguzi mkuu.
Seif Mangwangi Mratibu wa Arusha Press Club na Afisa mpango wa mradi huo
alisema kuwa miongoni mwa malengo ya kikao hicho ni kupitia
mafanikio,changamoto pamoja na matarajio ya baadae ya mradi toka ulipoanza
Machi 2019.
Alisema pia wanakikundi wanatakiwa kutunga kanuni zao ambazo zitakuwa
kama mwongozo zitakazosimamia kundi hilo la waandishi wa habari za mtandaoni.
Seif alisema kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa utetezi na
ushawishi wa haki za binaadam kwa kutumia takwimu(DDA)kupitia vyombo vya habari
mubadala(Altenartive media) unaofadhiliwa na mfuko wa maendeleo wa watu wa
marekani kupitia taasisi za freedom house pamoja na PACT na una simamiwa na
club ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha.
0 Comments