Nyumba ya Mwandishi wa habari wa kujitegemea Joctan Maganga baada ya kuharibiwa na wananchi. |
JESHI
la polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu saba ambao ni wakazi wa kata ya
Mwanga Kusini ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma kwa tuhuma za
kufanya fujo na uhalibifu wa nyumba pamoja na uporaji wa vitu mbalimbali
vyenye thamani .
Kamanda
wa polisi mkoani hapa ACP James Manyama alieleza tukio hilo lilitokea hivi
karibuni kuwa chanzo chake ni wananchi kumtuhumu Joctan Maganga ambaye ni
mwandishi wa habari wa kujitegemea kuhusika katika upoteaji wa
jirani yake Philipo Hussein mwenye umri wa miaka 21.
Ndugu wa kijana huyo ambaye anaelezwa
kupotea kwa takribanii siku saba wanaeleza kuwa kulikuwa na
mahusiano ambayosi mazuri kati ya kijana huyo pamja na Jocta Maganga amabye
anatuhumiwa kumteka ambapo inasemkana walikuwa wakigombania mpaka wa ardhi kwa
zaidi ya mwaka sasa hapo awali.
Aidha
katika tukio hilo askari wawili wa jeshi la polisi mkoani hapa walijeruhiwa
wakati wakijaribu kuzuia vurugu na uharabifu wa nyumba ambayo vitu
mbalimbali viliibiwa na wanannchi wenye asira kali.
Katika
hatua nyingine jeshi la polisi mkoani hapa lilimkamata mtuhumiwa mmoja mwanaume
ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa na silaha moja ain ya AK-47 ikiwa na
magazine moja yenye risasi 30 katika kata ya kalinzi wilaya ya kigoma
vijijini.
0 Comments