Baadhi ya wazee wilayani Kibondo wakiwa na vifaa vya kuoshea magari walivyokabidhiwa na shirika la Help Age International. (Picha Na James Jovin) |
Vifaa vya kuoshea magari vilivyotolewa kwa wazee wilayani Kibondo kwa lengo la kujikwamua kiouchumi. ( Picha Na James Jovin) |
SHIRIKA la Help age International wilayani Kibondo mkoani Kigoma limetoa vifaa mbali
mbali vilivyogharimu zaidi ya shilingi milioni tano vitakavyowasaidia
wazee kuanzisha mradi wa kuosha magari na hivyo kujipatia kipato
kitakachowasaidia kujikimu katika maisha
Akizungumza
wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo Afisa Ujasiliamali wa Shirika la Help
age wilayani Kibondo bw. Elisante Kiraha alisema kuwa vifaa hivyo vimetolewa
kufuatia maombi ya Kikundi cha Uchumi cha Wazee Kibondo walioomba kuanzisha
mradi wa kuosha magari ili kujikimu kimaisha
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Kibondo bw. Fransis
Mkosamali na Katibu wa baraza hilo Bw. Gidion Menyo wameshukuru kwa msaada huo
na kwamba watahakikisha mradi huo unakuwa mkubwa na kusaidia wazee wote hasa
wale wenye mahitaji maalumu na wasio jiweza.
Nae
Kaimu Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Kibondo Bw. Jamhuri Kidumu pamoja
na Afisa Usatawi wa Jamii Bi Sophia Gwamagobe wamewapongeza wazee hao kwa
kuanzisha mradi ambao utawasaidia katika maisha lakini pia shirika la Help Age
kwa kuwa karibu na wazee siku zote.
0 Comments