Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati wa swala na baraza la Eid el-Adh’haa iliyofanyika kitaifa jijini Dar es salaam. |
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa wa amani na utulivu huku akibainisha kuwa kiongozi wa nchi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki.
Waziri Mkuu aliyasema
hayo siku ya jana (Ijumaa, Julai 31, 2020) wakati akishiriki swala na baraza la Eid
el-Adh’haa iliyofanyika kitaifa jijini Dar
es salaam.
“Naamini viongozi wa dini na kila mmoja tunaendelea kuliombea taifa hili
ili uchaguzi wa mwaka huu umalizike salama, tujiepushe na lugha za uchochezi,
tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa, tuzungumze kile
ambacho wananchi hawa utawatendea.”
Waziri Mkuu alisema kuwa kutokana na mfululizo wa matukio ya moto yaliyotokea katika taasisi za dini ya kislam ikiwamo Shule za Ilala Islamic na Kinondoni Muslim, Serikali kwa kushirikiana na vingozi wa dini hiyo wameanza uchunguzi ili kuibaini chanzo cha tatizo hilo.
“Hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria iwapo mtu yoyote atabainika
kuhusika na matukio haya ya moto katika taasisi za dini ya kiislam, kama
kulikuwa na dhamira ya mtu binafsi kuharibu miundombinu hii na kutia hasara kwa
njama,hatuwezi kumvumilia na kama kutakuwa na makosa ya mifumo tutafuatilia na
kufanya marekebisho makubwa.”
Alisema, Rais Dkt. John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan wanawatakia watanzania na waislam wote sikukuu njema ya Eid na amepokea salamu
za pongezi zilizotolewa kwa Serikali na
viongozi wa dini ya kiislamu namna Serikali inavyosimamia suala la amani nchini.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwataka waislam kujiepusha kutoa matamko ya mtu mmoja mmoja
yanayoweza kuwavuruga waislam wote bali waendeleze mshikamano na mahusiano kwa
waislam wote na taasisi nyingine
Naye, Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh
Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana aliwataka watanzania kutambua kuwa uchaguzi
mkuu ni wa watanzania wote, hivyo wanapaswa kuchagua viongozi wanaohitajika na
ambao wataweza kukidhi haja za watanzania.
“Hakuna haja ya vurugu,
ghasia wala kufanya fujo ya aina yoyote, tushikamane ili kuufanya uchaguzi
vizuri, tumalize vizuri na kuijenga nchi yetu kwani sisi sote tunatakiwa
tuijenge nchi.”
0 Comments