Magari maalum yaliyoandaliwa kwaajili ya kampeni ya kuhamasisha jamii kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona. (Picha Na Isaac Aron Isaac) |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Simon Chacha akikabidhi vipeperushi kwa baada ya wananchi watakaoshiriki kwenye kampeni hizo. (Picha Na Isaac Aron Isaac) |
WIZARA
ya afya kupitia kitengo cha elimu ya afya kwa umma imezindua rasmi kampeni ya
kuhamasisha jamii kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa
Corona kwa mikoa 14 nchi nzima kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa na
wataalamu wa afya na serikali.
Kampeni
hiyo inaelezwa kufika katika maeneo yote ya mikoa hiyo kwa siku 30 kwa kila
mkoa ambapo licha ya ugonjwa huo kuelezwa kupungua kwa kiasi kikubwa bado nchi
jirani zinakabiliwa na ugonjwa huo hivyo kuendelea kuhamasisha jamii kuchukua
tahadhari.
Dkt
Hamesha Chinyuri kutoka idara ya kinga kitengo cha elimu ya afya kwa umma
anasema kwamba kampeni hiyo itaendeshwa kiupitia magari maalum ambayo yatakuwa
yanapita katika mitaa mbalimbali kuendelea kutoa elimu.
Akizundua
kampeni hiyo kwa Mkoa wa Kigoma Mganga mkuu mkoani hapa ameeleza kuwa kampeni
hiyo itakuwa chachu ya kusaidia wananchi kuendelea kujikinga na magonjwa
mengine ikiwemo ugonjwa wa malaria ambao umekuwa na kiwango kikubwa cha
maambukizi mkoani Kigoma.
Katika
kampeni hiyo wizara ya afya kupitia kitengo cha elimu kwa umma inashirikilia na
shirika la msalaba mwekundu katika kutoa elimu ya uhamasishaji kwa wananchi
kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona.
0 Comments