CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA YAWAATHIRI WAKAZI UVINZA

 

Naibu waziri wa Ujenzi Mhandisi Elias Kwandikwa akikagua ujenzi wa barabara ya Simba Kalya mara baada ya kutembelea vijiji hivyo. (Picha NA Isaac Aron Isaac)

Baadhi ya wananchi wa Vijiji vya Simbo Kalya wakiendelea na shughuri zao kwa kutumia barabara ambayo inaendelea kujengwa. (Picha Na Isaac Aron Isaac)

Barabara ya Simbo Kalya inayojengwa kwaajili ya kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa vijiji hivyo. (Picha Na Isaac Aron Isaac)

Na Isaac Aron Isaac, Kigoma

Wakazi wa  vijiji vya kusuni mwa ziwa Tanganyika Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wameiomba serikali kufanya marekibisho ya miundombinu ya usafiri kuelekea katika vijiji hivyo ili kuepuka adha pamoja na vifo vitokanavyo na changamoto ya usafiri.

Wameeleza hayo katika ziara ya Naibu waziri wa Ujenzi Mhandisi Elias Kwandikwa alipotembela barabara ya Simbo Kalya yenye urefu wa kilometa takrabini  230 ambayo licha ya kujengwa kwa kiwango cha vumbi bado imekuwa na tatizo kwa wananchi wa meneo hayo.

Kwa mujibu wa wananchi hao kuanza Mwezi Januari mwaka huu vifo kadhaa vimeripotiwa mpaka sasa  katika  ziwa Tangayika kwa upande wa kusini ambapo wakazi wake wanaeleza kuwa ni kutoka na  changamoto ya usafiri ambayo imekuwa  ikiwalazimu kupanda maboti ambayo si salama kwa uhai wao.

Aidha Meneja wa Tanroad mkoani Kigoma Mhandisi Narsisi Choma ameeleza kuwa kwasasa ukarabati unaendelea katika maeneo ambayo yaliingiliwa na maji kutoka ziwani ambapo tayari serikali imetoa fedha kwaajili ya  ujenzi barabara katika kijiji cha Sibwesa ambapo kuna changamoto kubwa zaidi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mhandisi Elias Kwandikwa aliwatoa hofu wakazi wa maeneo hayo na kusisitiza kuwa maboresho hayo ya yatahusisha ujenzi kwa kiwango cha Rami ili kusaidia pia katika shughuli za kiuchumi na kibiashara katika maeneo hayo ambayo shughuri za kimaendeleo zinakwama kutokaa  na ubovu wa barabara.

Hata hivyo Barabara ya Simbo Kalya ilianza kujengwa mwaka 2012 chini ya Tanroad baada ya kutokuwepo hapo awali lakini bado  wananchi  wa maeneo hayo wanaeleza kuwa wao hujisikia amani zaidi wakipanda usafiri wa majini zaidi ya barabara.

 


Post a Comment

0 Comments