HAKI HAIPOTEI, MILIONI 54 ALIZODHULUMIWA MIAKA 6 ILIYOPITA ZARUDISHWA

 

                               bi. Evodia Pius mhanga wa wizi huo (picha na James Jovin )


 

KAKONKO

 

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilayani Kakonko mkoani Kigoma imefanikiwa kurudisha fedha kiasi cha shilingi milioni 54 za  mwalimu mstaafu alizokuwa amedhulumiwa na mkopesha liba miaka sita iliyopita

 

Kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani kakonko bw. Ladislaus Ibrahimu akizungumza na KGPC Blog  amesema kuwa aliyekuwa ameibiwa ni bi. Evodia Pius aliyekuwa akifundisha shule ya msingi Kasanda baada ya kukabidhi kadi ya benk kwa mkopesha liba aliyeamua kuhamisha fedha hizo kiasi cha shilling milioni 54

 

Amesema kuwa bi. Evodia alistaafu kazi mwaka 2014 na kupewa pensheni ya milioni 70 lakini baada ya kustaafu alidanganywa na mkopesha liba ambaye hakutajwa jina lake ambaye alimkopesha kiasi cha shilingi milioni saba ili aweze kujenga nyumba kisha akamuibia mama huyo kiasi cha shilingi milioni 54 katika akaunti yake ya benki na kuzihamishia katika akaunti yake binafsi

 

Aidha bi. Evodia ambae alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Kasanda amesema kuwa aliyesaidia kupatikana kwa fedha hizo ni mwanae wa kike ambaye wakati zinaibiwa alikuwa bado mdogo na ndipo baada ya miaka sita kupita alipata ufahamu na  aliamua kuomba msaada kwa mkuu wa wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagara ambaye baadae aliagiza taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU kufuatilia sakata hilo na waliweza kufuatilia kwa kina na kugundua kuwa fedha hizo ziliibiwa na mtu aliyekuwa amemkopesha mama yake kwa liba miaka sita iliyopita.

 

Mkopeshaji liba huyo ambaye hakutajwa jina lake kwa sababu za kiusalama alikili kufanya hivyo na ndipo ameweza kutoa shilingi milioni kumi za awali na fedha zote zilizobaki atazilipa kila mwezi na kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2020 ameahidi atakuwa amemaliza kurudisha fedha zote mali ya bi. Evodia

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kakonko kuendesha semina kwa wafanyakazi wote juu ya tatizo hili la mikopo ya liba linaloendelea kushamili kila siku huku watumishi walio wengi hasa wastaafu wakiibiwa fedha zao kila kukicha. ENDS 

 

 

 

 


Post a Comment

1 Comments

  1. Wamefanya jambo la kheri Mungu amsaidie sana bi evodia na wafanyakazi wengine yujifunze mikopo.hiyo isio salama

    ReplyDelete