Maafisa wa Kampeni ya Utoaji Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati walipomtembelea kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuanza kwa zoezi la utoaji elimu kwa Mlipakodi (mlango kwa mlango) mkoani hapo. |
Na Magreth
Magosso,Kigoma
MAMLAKA ya
Mapato (TRA) imetambulisha Kampeni ya utoaji Elimu kwa Mlipa kodi
ya Mlango kwa Mlango kwa Mkuu wa Mkoa Thobiasi Andengenye ikiwa ni kampeni
itakayo dumu kwa wiki mbili katika halmashauri za mkoa huoa.
Akitambulisha
Kampeni hiyo leo katika ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa, Meneja wa TRA
Kigoma Jacob Mtuman'gombe alisema lengo ni kuwafikia wafanyabiashara kwa
urahisi kuliko semina zilizozoeleka ambapo wengi hawafiki kupata elimu sahihi
ya ulipaji kodi.
"Vigumu
walipa kodi kufunga maduka na kuja kwenye semina, zoezi la mlango kwa
mlango ni fursa ya kupanua uelewa kwao na wao kutupa changamoto zao na kutathimini
ufanyaji kazi wao hivyo nawasihi wasikimbie wahusika wapo kwa ajili ya
kuwaelimisha na si vingine" alisisitiza Mtuman'gombe.
Alisema timu
ya maofisa elimu ya mlipaji kodi kutoka makao makuu watashirikiana na maofisa
wa mkoani humo ikiwa ni moja ya mkakati wa mamlaka katika kurahisisha zoezi la
utoaji wa elimu kwa wadau wao ndio sababu ya kuomba ridhaa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma ili abariki zoezi hilo litakalo dumu kwa wiki mbili katika wilaya
mtambukwa kwa maslai mapana ya jamii na Taifa kiujumla.
Aidha amekiri
zoezi hilo kuwa chachu kwa wakwepa kodi kutambua wajibu wao na mamlaka kubaini kero
zao kwa kutathimini biashara zao kwa malipo stahiki ya kodi.
Akipokea
ombi hilo Mkuu wa mkoa huo Tbobias Andengenye alisema atahakikisha taasisi zote
zinawapa ushirikiano kwa lengo la kuboresha ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla
.
.
"Siku
zote ukitumia nguvu kudai haki haisaidii zaidi ya migogoro lakini kitendo cha
kumpa elimu sahihi Mwananchi ni chachu ya mabadiliko tarajiwa hivyo tumieni
elimu hiyo kwa matokeo chanya"alisema.
Aidha
Andengenye amewakumbusha maofisa wa TRA kutumia vyema sheria ya kodi kwa hekima
na busara ili kuondoa mikwaruzano baina ya wafanyabiashara na serikali
huku akitolea mfano wa baadhi ya wafanyabiashara kuacha kuratibu bidhaa zao hapa
mkoani na kwenda mikoa jirani kuratibu bidhaa hizo jambo ambalo ni dalili
ya shida ya tafsiri ya sheria ya ulipaji kodi.
Alishauri
kutoza kodi kwa weledi ili kuwapa fursa wafanyabiashara wadogo wakati na
wakubwa kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya nchi ambayo inategemea fedha za
ndani kukamilisha miradi husika.
Akizungumza
na Kgpc blog mfanyabiashara wa Soko la kigoma mjini Prisca David alikiri
TRA haina shida na mtu endapo utakuwa na leseni ya biashara, Mashine ya kieletroniki ambayo inatoa risiti
kulingana na mauzo na kushauri
wanaotumia njia za panya waache.
Naye
Deudatius Vuma mfanyabiashara soko la kigoma mjini alisema kitendo cha TRA
kuwafuata wadau wao ni la kupongezwa na si la kubezwa huku akiongeza kuwa nchi
inaenda kwa kasi katika kuboresha huduma za jamii katika miradi ya Umma hivyo wafanyabiashara
wawe wakweli katika biashara zao.
0 Comments