Na James Jovin
KIBONDO
Halimashauri
ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma iko katika hatua za mwisho za umaliziaji wa
kituo cha afya katika kata ya Nyaruyoba kituo ambacho kitaghalimu zaidi ya milioni mia tatu mpaka kukamilika
kwake ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuboresha huduma za afya
Hayo yamebainishwa
na Dr. Laurian Kanaganwa wakati
akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo katika
ukaguzi wa shughuli hiyo na kwamba ujenzi umefikia asilimia tisini mpaka sasa
Aidha amesema
kuwa kukamilika kwa kituo hicho cha afya kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
vifo vya akina mama na watoto vilivyokuwa vikitokea kutokana na ukosefu wa
huduma za afya na kutembea umbali mrefu katika kutafuta matibabu
Katika hatua
nyingine Dr. Kanaganwa amesema kuwa mradi huo wa kituo cha afya unatekelezwa
kwa kutumia force account na unatarajiwa kumalizika ndani ya miezi mitano,
mpaka sasa mradi huo umeghalimu fedha za kitanzania million 239.7 ambapo salio
ni shilingi milioni 60.2 wakati ujenzi umefikia asilimia 90
Nao baadhi
ya wananchi wa kata ya Nyaruyoba wameipongeza serikali kwa hatua hiyo na kwamba
walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma katika kituo cha
afya Kifura au hospitali ya kibondo hivyo kukamilika kwa kituo hicho ni hatua
kubwa ya maendeleo katika kata yao. ENDS
0 Comments