WAZIRI MKUU MAJALIWA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE

 

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Ruangwa mkoani Lindi na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa Bw. Frank Chonya.


Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akionyesha fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Ruangwa mkoani Lindi.




Na Mwandishi Wetu, Lindi


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Leo Agosti 21, 2020 amechukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Ruangwa Katika mkoa wa Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

Waziri Mkuu amekabidhiwa foam hiyo katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa Bw. Frank Chonya.

 

Baadaya tukio hilo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alishiriki sala ya Ijumaa na waumini wa Dini ya Kiislam katika msikiti wa Nnur uliopo wilayani Ruangwa.

 

Post a Comment

0 Comments