ZIMAMOTO KIGOMA "WANANCHI WASISEME UONGO KUTUHUSU"



Na Isaac aron Isaac

Jeshi la zimamoto Mkoani kigoma limekanusha madai ya baadhi ya wananchi mkoani humo kuwa jeshi  hilo halina vifaa vya kutosha katika kufanya shughuli za uokoaji pindi matukio mbalimbali yanapojitokeza.

Hayo yamezungumzwa na kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi Abdalah Maundu na kusisitiza kuwa jeshi  hilo liko imara kuwahudumia wananchi na vifaa vyote vipo kulingana na uhitaji.

  Maundu amesema  lalamiko kubwa ambalo wanapata kutoka kwa  wananchi ni ujazo mdogo wa maji ambao hutumika katika kuzima moto katika matukio kadhaa na kuwafanya baahdi ya wananchi kukosa imani na utendaji kazi wa jeshi hilo.

Amesisitiza kuwa jeshio hilo hufabnya kazi wka uataribu maalumu kulinga na vifaa vilivypo ambapo kw asasa gari lililopo ambalo hutumika kuwhaudumia wananhcio nio moja huku ujazi wake ukiw ani liota 1500 hivyio kulaizmika kujazwa kila wakat pale ambapo tukio huhityaj maji mengi zaidi.

Kwa sasa jeshi hilo lina magari matatu mkoa mzima ambapo moja lipo uwanja wa ndege lingine lipo manispaa ya kigoma ujiji huku lingine likiwa limeharibika kusubili matengenezo ambapo jeshi hilo limesisitiza kwamba liko imara kutoa huduma kwa wananchi

Katika kipindi cha uchaguzi na kampeni jeshi la zimamoto mkoani Kigoma limesisitiza kuwa liko tayari kuwahudumia wananchi katika  matukio mbalimbali yanapojitokeza na kuwataka kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa za matukio pindui yanapotokea.

 Kwa mujibu wa melezo ya kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoji mkoani Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi Abdalah Maundu amesema jesho hilo lina magari matatu ya uokoaji ambapo mpaka sasa mawili pekee ndio hufanya kazi kwa mkoa mzima wa kigoma.

MWISHO.

 

jknj
Kamanda wa jeshi la zimamoto mkoani Kigoma Kamishna msaidizi mwandamizi Abdalah Maundu akizungumza na waandishi wa habari.(Picha na Isaac Aron Isaac)

Moja kati ya magari ya uokoaji katika jeshi la zimamoto mkoani Kigoma
(Picha na Isaac Aron Isaac)


AAAAAA
Askari wa jeshi la zimamoto Mkoan Kigoma wakionyesha namna ya kuzimamoto ikiwa ni moja ya sehemu ya mazoezi yao (Picha na Isaac Aron Isaac)


Post a Comment

0 Comments