MKINICHAGUA UCHUMI WA WILAYA YA BUHIGWE UTAPAA-PHILIPO MPANGO

 

Mgombea ubunge wa jimbo la Buhigwe kupitia chama cha mapinduzi Dkt Philipo Mpango ambaye pia ni waziri wa fedha na mipango akiongea na wananchi kata ya mnanila wakati wa uzinduzi wa kampeni zake leo.




Na Editha Karlo,Buhigwe

MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Buhigwe kupitia chama cha mapinduzi(CCM)Dkt Philipo Mpango ambaye pia ni waziri wa fedha wa awamu ya tano amewataka wananchi wa Wilaya ya Buhigwe octoba 28 kumchagua kuwa mbunge wao kwani atafanya kazi kubwa ya kuhakikisha uchumi wa Wilaya ya Buhigwe unakuwa kwa kasi na Wilaya hiyo inasimama vizuri katika maendeleo.


Mpango ameyasema hayo leo kwenye viwanja vya soko la mnanila wakati akizindua kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.


Mpango amewaomba wananchi wa kata ya Mnanila kukichagua chama cha mapinduzi(CCM)ili iweze kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara inayounganisha nchi jirani ya Burundi na Mikoa ya Kigoma,Kagera na Geita pamoja na kuboresha barabara za ndanu ili kuwezesha wananchi kusafirisha mazao yao katika maeneo yenye masoko.


Amesema pamoja na mradi huo wa barabara wenye urefu wa kilometa 260 pia serikali itajenga stand mpya ya mabus manyovu,pia watajenga shule ya kisasa ya kidato cha tano na sita kwaajili ya wanafunzi wanaofauli masomo yao.


Mgombea huyo amesema kuwa miaka mitano ijayo ilani ya chama imeelekeza kuhakikisha wanapata tija katika mazao yao na vijiji vyote ambavyo havina umeme na maji vinapata huduma hiyo ili kufanikisha mpango wa serikali ya CCM ambapo hadi kufikia mwaka 2025 Tanzanua inakuwa nchi ya kuigwa barani Afrika.


Uzinduzi wa kampeni hizo umehudhuriwa na umati wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Buhigwe,wagombea ubunge wa Mkoa wa Kigoma wote 

wa  Mkoa wa kigoma walijitokeza kumsindikiza Dkt Mpango katika uzinduzi huo.


"Mkinichagua nikiwa mbunge wenu nina wahakikishia kuwa nitafanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali pamoja na chama changu ili kuhakikisha maendeleo katika Wilaya yetu ya Buhigwe yanakimbia na uchumi wa Buhigwe lazima ubadilike"alisema Dkt Mpango


"Mungu ametupa akili,ardhi nzuri wana Buhigwe ambayo tunalima mazao mengi Naomba mnitume mimi mtumishi wenu niweze kutafuta masoko ya mazao pamoja na viwanda ili kuongeza thamani ya mazao yenu ambapo mtaboresha vipato vyenu"alisema


Alisema Wilaya ya Buhigwe ni miongoni mwa Wilaya mpya hivyo inahitaji vitu vingi vya maendeleo kwa haraka.


"Hii Wilaya yetu ni mpya inahitaji vitu vingi ili maendeleo yakue kwa haraka hapa tunatakiwa tupate mahakama nzuri yenye hadhi ya Wilaya yetu,huduma za afya pamoja na elimu naomba mimi pamoja na madiwani wote wa CCM ili nifanye nao kazi ya kuwaletea maendeleo"


Naye Mgombea ubunge kupitia viti maalum(UWT)Mkoa wa Kigoma Zainabu Katimba amewataka wana buhigwe kuchagua mafiga matatu ambayo ni Rais,Mbunge na madiwani wa CCM ili waweze kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wanabuhigwe kwa kushirikiana.


"Tarehe 28 octoba ndugu zangu msifanye makosa msichanganye rangi chagueni rangi moja tu rangi ya kijani kwenye jimbo hili la buhigwe tupate ushindi wa kishindo katika jimbo hili"alisema


Post a Comment

0 Comments