Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Polisi Thobias Andengenye |
Na Isaac Aron Isaac, Kigoma
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina wa polisi
(CP) Thobias Andengenye ameeleza kutoridhishwa na ujenzi wa shule ya msingi ya
mfano ya Bwega inayojengwa wilayani Buhigwe mkoani kigoma kwa gharama ya
shilingi million 700.
Awali ujenzi wa shule hiyo ulipigiwa kelele na
waziri wa elimu Prof Joyce Ndalichako alipotembelea mradi huo mwezi October
mwaka jana kwa kushindwa kufuata taratibu za ujenzi ambapo pia aliagiza
kurekebishwa kwa ramani lakini hadi sasa suala hilo halijafanyiwa kazi.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa vyumba 17 vya
madarasa ambapo kwa sasa ujenzi wake unaendelea licha ya kupigiwa kelele
na viongozi kadhaa kwa kushindwa kuendana na hali halisi ya ujenzi wa majengo
ya shule za serikali.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma CP Thobias Andengenye
naye akasisitiza ramani ya ujenzi wa vyumba vya ofisi ya waalimu na jengo la
jiko kuerekebishwa kabla ya wanafunzi kuanza kupata huduma katika shule
hiyo.
“Ofisi ya walimu inatakiwa kuangalia madarasa
ili wanafunzi kuwa na nidhamu muda wote wakijua waalimu wanawatazama, huwezi
kujenga ofisi ya Mkuu wa Shule ambayo imeyapa mgogo madarasa” alisema Mkuu wa
Mkoa Andengenye
0 Comments