Na Emmanuel Matinde, Kigoma
Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini, TASAF,
kipindi cha kwanza cha awamu ya tatu, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma,
wamesifu mpango huo ulivyosaidia kuwatoa katika hali ya umasikini uliokithiri
na kuweza kuboresha hali yao ya maisha.
Lonka Musa Lonka na Anezia Benedicto wakazi wa Kijiji cha
Mkongoro katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma, ni baadhi ya walengwa
walionufaika na mpango wa TASAF, na walieleza kuwa awali walikuwa na maisha
magumu ila baada ya kupokea pesa walianza kujenga na sasa wanaishi kwenye
nyumba nzuri.
“Wakati wa mvua tulikuwa tunapata shida sana kutokana na nyumba
kuvuja, lakini kwasasa tunaishi kwenye nyumba nzuri na watoto wanaeda shule
bila kuwa na madeni ya ada, tunaishukuru sana TASAF kwa kutubadirilishia maisha”
walisema
Abihudi Abeli ni Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Mkongoro,
wao wamezungumzia mabadiliko aliyoyashuhudia kwa walengwa wa TASAF kijijini
hapo, huku Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Angela Petro akieleza kuwa elimu
iliyotolewa kwa walengwa kabla kupokea ruzuku ya TASAF, imesaidia fedha
kutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Awali watu walikuwa nakosa hata mlo
mmoja kwa siku lakini baada ya TASAF watu wanakula kuanzia milo miwili hadi
mitatu inategemeeana na jinsi mtu alivyojipanga kupitia ile pesa aliyoipata
kupitia mfuko wa TASAF” alisema.
Kijiji cha Mkongoro kina watu zaidi ya elfu kumi na tatu, ambapo
mpaka sasa wanufaika wa mpango wa TASAF ni 205.
0 Comments