Na
Tryphone Odas, Kigoma
Mkuu
wa Mkoa Kigoma, Kamishna wa Jeshi la Polisi,
Thobias Andengenye amewataka wafanyabiashara wa Mkoa huu kurasimisha
biashara zao kwa wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ili kila mfanyabiashara
aweze kufanya biashara bila kusumbuliwa na kudhibiti biashara ambazo sio rasmi.
Amesema
hayo wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Biashara wa Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi
yaliandaliwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni Brela yakilenga kuwajengea
uwezo wa namna ya kusajili biashara za wafanyabiashara kwa njia ya mtandao.
“Watu
wamekuwa na hofu ya kuanzisha biashara kutokana na mambo mengi wanayotakiwa
kuyafanya hivyo serikali kwa kuliona hilo na kupitia BRELA imeamua kurahisisha
jambo hili ili kumfanya mtu mwenye nia ya kufanya biashara aweze kufanya
biashara” alisema Kamishina Andengenye.
Mkuu wa Mkoa Kigoma, Kamishna wa Jeshi la Polisi, Thobias Andengenye. (Picha na Tryphone Odace) |
Afisa Rasilimali watu kutoka Wakala wa Usajili Biashra na Leseni Bw. Migisha Kahangwa alisema mfumo huo utasaidia wafanyabishara kuondokana na usumbufu wa kutumia gharama kubwa kwenda kutafuta hudama za usajili.
“Lengo
ni kulasimisha biashara na kuwawezesha wananchi kupunguza gharama na kuweza kuwa
rasmi katika kuendesha biashara zao” aliongeza Bw. Kahangwa.
Kwa
upande wake Afisa Biashara wa Mkoa wa Kigoma, Deogratias Sangu, alisema mfumo
huo utasaidia wafanyabiashara wengi kujisajili kwani kuondoa wimbi la wafanyabiashara
ambao sio rasmi kutokana na mkoa huu kupakana na Nchi nyingine.
Baadhi
ya maafisa biashara akiwemo Bi. Imelda Ukololo
na Godfrey Selestine walisema kwa kipindi cha nyuma hawakuwa na uwezo wa
kusajili viwanda kwa mfumo wa kawaida na hivyo mafunzo hayo yatawasaidia
kuboresha na kutoa leseni zinazopatikana kwa njia ya mtandao kwa urahisi.
0 Comments