Hospitali ya wilaya ya Kokonko inayojengwa katika kijiji cha Itumbiko. |
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanal Hosea Ndagala akizungumzia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kakonko.( Picha Na Mwajabu Hoza) |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Stephano Mag'hanila. |
Na Mwajabu Hoza , Kakonko - Kigoma
WAKAZI zaidi la laki mbili wa wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wanatarajia kunufaika na ujenzi wa mradi wa Hospitali ya wilaya mradi ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.5.
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya hiyo Kanal Hosea
Ndagala amesema Ujenzi huo unatekelezwa katika Kijiji cha Itumbiko ndani ya
wilaya ya Kakonko ambapo hadi sasa umefikia katika hatua nzuri za ujenzi
wake.
Aidha hadi sasa majengo yanayoendelea na ujenzi ni pamoja na jengo la nje OPD pamoja na Maabara ambapo mradi huo wa majengo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 500.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kakonko Stephano Mag'hanila amesema kukamilika kwa majengo hayo itakuwa chachu ya ukuaji wa maendeleo ya wilaya hiyo ambapo mradi huo utaongeza uwekezaji mkubwa wa majengo ya kulala wageni pamoja na kukuza ajira kwa vijana wa wilaya ya Kakonko .
´´ Mradi huu wa hospitali ya wilaya utatoa
fursa kwa wakazi wa ndani, wa nje na wakazi wa wilaya jirani ambapo
hospitali itapokea wagonjwa wa rufaa kutoka nje na hivyo utatoa fursa ya
ukuaji wa uchumi wa wilaya kwa kuwa kutakuwa na uwekezaji wa nyumba za
kulala wageni kwa ajili ya watu watakaokuwa wanahudumia wagonjwa wao ´´
alisema Stephano.
Jengo la OPD katika Hospitali ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma inayojengwa katika kijiji cha katika kijiji cha Itumbiko. |
Jengo la maabara katika Hospitali ya Wilaya ya Kakonko inayojengwa katika kijiji cha katika kijiji cha Itumbiko. |
0 Comments