WAZIRI MAJALIWA: HAKUNA RAIS ZAIDI YA DKT MAGUFURI

Waziri Mkuu wa Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akiwa akiwa katika mkutano na wananchi wa Butiana mkoani Mara, pembeni ni mama Maria Nyerere. 


Na Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM amesema kati ya wagombea urais waliojitokeza, hakuna kiongozi zaidi ya Dkt. John Pombe Magufuli. 

 

Alitoa kauli hiyo siku ya jana (Jumamosi, Septemba 19, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Butiama, wilayani Butiama, kata za Nyamuswa na Mugeta wilayani Bunda, akiwa njiani kuelekea Mugumu, Serengeti, mkoani Mara.

 

“Nimekuja kuomba kura kwa ajili ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ili apate miaka mitano mingine kwa sababu hakuna kiongozi bora kati ya wote waliojitokeza zaidi ya Dkt. John Pombe Magufuli.

 

“Wanaokuja kuomba uongozi ni wengi lakini hakuna chama chenye benki ya viongozi kama CCM. Hakikisheni mnatupatia viongozi wa CCM ili waweze kufanya kazi pamoja na kwa kuelewana.”  alisema.

 

Aidha Waziri Majaliwa alitumia mikutanohiyo kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Bunda, Bw. Boniface Chacha Getere, wagombea udiwani wa wilaya zote mbili za Butiama na Bunda.

 

Alisema uongozi ni lazima utengeneze timu inayofahamiana na inayozungumza lugha moja “Chama cha Mapinduzi kimeleta viongozi watatu safi. Kwa hiyo ukienda kupiga kura chagua hao watatu ambao ni mgombea urais, ubunge na udiwani.”  

 

 

 


Post a Comment

0 Comments