Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya ziara ya kikazi
liyoanza jana tarehe 2 Septemba 2020. |
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi
liyoanza jana tarehe 2 Septemba 2020. |
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Kagera
Waziri wa Kilimo
Japhet Hasunga jana Septemba 2, 2020 amewasili Wilayani Bukoba katika
mkoa wa Kagera ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya ziara ya
kikazi katika Wilaya ya Bukoba, Kyerwa, Karagwe na maeneo mengine mahususi
yanayojishughulisha na kilimo hususani zao la Kahawa.
Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia na
kujionea hali ya malipo ya wakulima wa kahawa wanaodai, kukutana na viongozi wa
vyama vya Ushirika na kufanya mikutano ya kuwasikiliza wananchi kuhusu
changamoto zinazowakabili katika sekta ya kilimo.
0 Comments