Mkurugenzi mkuu wa Ofisi
ya Taifa Takwimu (NBS)Dkt Albina Chuwa (kushoto) na Meneja wa Majengo TBA Mkoa wa Kigoma Julias Chego wakibadirishana
nyaraka baada ya kutiliana sahini ya mkataba wa ujenzi wa ofisi ya Takwimu Mkoa
wa Kigoma, anaye shuhudia katika ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye.
Na Tryphone Odace, Kigoma
Serikali
imetoa zaidi ya Shilingi Milioni
600 kwa ajili kukamilisha ujenzi wa jengo la
Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Kigoma, baada ya kukaa kwa zaidi ya
miaka 26 bila kukamilika tangu lilipoanza kujengwa mwaka 1994.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu NBS, Dkt Albina Chuwa, alisema hayo wakati wa hafla fupi ya ya
kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa ofisi hiyo na Wakala wa Majengo nchini TBA.
Kwa upande wake Meneja wa TBA, Mkoa wa Kigoma Julius Daniel, ambao wamepewa miezi
miwili tu kukamilisha kazi hiyo, aliahidi kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
Hafla hiyo ya kutiliana saini
ilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andngenye, ambaye kwa upande
wake aliwataka wananchi kutumia takwimu katika ngazi ya familia kwa maendeleo
ya familia zao.
0 Comments