ALIYEMLAWITI MTOTO WA MIAKA 12 KUTIWA NGUVUNI

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Jeshi la Polisi Thobias Andengenye

 

Na Tryphone Odace

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Jeshi la Polisi Thobias Andengenye ameiagiza polisi kumkamata na kufuta dhamana ya mwanaume anaekadiriwa kuwa na  umria  wa miaka 60 anaetuhumiwa kumlawiti  mwanafunzi  wa darasa la nne mwenye umri wa miaka  12.

Alitoa  agizo  hilo wakati  akizungumza na waandishi wa habari waliomtaka aingilie kati na kuona namna ya kukomesha vitendo vya ulawiti, ubakaji na matukio mengine ya ukatili hususani kwa wanawake na watoto ambayo yamekuwa yakiripotiwa  bila hatua kuchukuliwa.

Tukio la mwanafunzi huyo kulawitiwa lilitokea mwezi Septemba mwaka huu na kuripotiwa kituo kikuu cha polisi mkoani hapa Octoba 26, huku sababu ya kuchelewa kuripotiwa ikielezwa kuwa ni baada ya mtuhumiwa kumtishia maisha mwanafunzi huyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Alchelaus Mutalemwa amekiri kuripotiwa kwa tukio hilo na kuahidi kulifanyia kazi agizo la Mkuu wa mkoa haraka iwezekanavyo.

 

 

 

 

 

 


Post a Comment

0 Comments