BEI YA SARUJI YAPANDA KWASABABU YA USAFIRISHAJI KIGOMA



Na Isaac Aron Isaac

WAFANYABIASHARA wa saruji mkoani Kigoma wameeleza sababu za kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kuwa ni kutokana na changamoto ya usafirishaji kwa njia ya treni kutoka kiwandani ambao husababisha ucheleweshaji wa bidhaa hizo sokoni.

Walieleza hayo katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina wa Jeshi la polisi Thobias Andengenye alipotembela maduka ya wauzaji wa jumla na lejaleja wa bidhaa hiyo katika manispaa ya Kigoma ujiji ili kujua hali ya ununuzi na uuzaji wa saruji.

Wafanya biashara hao walisema kuwa kwasasa wanauza mfuko mmoja kwa shilingi elfu 21 mpaka 22 ambapo licha ya bidhaa hiyo kuwa hafifu kiwandani bado changamoto kubwa inayosababisha kupanda kwa gharama ni kutoka na usafirishaji wake kutoka Dar Es Salaam.

Akizungumza baada ya kutembelea maduka hayo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa jeshi la polisi Thobias  Andengenye alisema uongozi wa mkoa utafanya kila jitihada ikiwemo kuzungumza na Shirika la Reli Tanzania TRL ili kuwa na mpango maalumu wa usafirishaji wa mizigo kuja mkoani Kigoma.

Kwa sasa hali ya upatikanaji wa saruji kwa mkoa wa Kigoma uko chini zaidi na kusababisha  baadhi ya maduka ya bidhaa hizo kufungwa huku mengine yaliyobaki yakiwa na idadi ndogo tofauti na kawaida.

 

 

Post a Comment

0 Comments