Na Emmanuel Matinde
Mzee anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka 70 mkazi wa Mlole kwa jina Jumanne Rashid, amefariki
dunia baada ya kuangukiwa na jiwe kubwa wakati akichimba madini ujenzi katika
eneo la wachimbaji wadogo wa madini hayo yaliyopo eneo la Masanga Manispaa ya
Kigoma Ujiji.
Mkuu wa Kitengo cha
Ukaguzi Kinga na Tahadhari za Moto katika jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa
Kigoma, Sajenti Bahati Salum, kwa niaba ya Kamanda wa Mkoa wa Kigoma wa Jeshi
hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi Abdallah Maundu, amethibitisha tukio hilo.
“Tulifika eneo la
tukio baada ya dakika 15 na tulikuta kweli mwananchi huyo amefukiwa, hatua
tuliyoichukua ni kuwasiliana na jeshi la polisi ambao walituruhusu kuchukua
mwili na kuupeleka katika hospitali ya mkoa maweni na hatua zaidi
zitachukuliwa pale” alisemaa Sajenti Salumu.
Miongoni mwa
walioshuhudia tukio hilo lililotokea jana majira ya saa tisa alasiri ni Hamisi
Jonas ambaye pia ni mchimbaji wa madini ujenzi katika eneo hilo la Masanga
alisema, “kabla ya tukiwa tulikuwa tunazungumza na yule mzee na baada ya
mazungumzo kila mmoja aliendelea na kazi ila baada ya muda tena nilisikia mawe
yakidondoka kwa kishindo na nilipoenda kuangalia nikakuta yule mzee ameangukiwa
na jiwe
Aidha Sajenti Bahati
Salum, aliwataka wachimbaji katika eneo hilo wawe waangalifu katika kipindi
hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha au wasimamishe kabisa shughuli za
uchimbaji hadi pale mvua zitakapomalizika.
0 Comments