DEO NSOKOLO AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA RAIS UTPC

 


MATOKEO ya uchaguzi wa Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) yamempa ushindi wa kishindo Deogratius Nsokolo ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma huku akiwa amechukua nafasi hiyo kwa mara nyingine tena.

 

Nsokolo amepata kura 72 katika kura 83 ziliopigwa na wajumbe 83 huku mpinzani wake Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza akipata kura 11 pekee.

 

Matokeo hayo yanampa nafasi Deogratius Nsokolo kutumikia nafasi ya Urais wa UTPC kwa miaka mingine mitano kuanzia 2020-2025 ambapo awali alitumika katika nafasi hiyo mwaka 2015-2020.

 

Matokeo kwa ujumla haya hapa:

 

Wagombea wanawake

Walioshinda nafasi ya ujumbe wa bodi ya wakurugenzi UTPC ni

1. Hadija Omar 48

2. Lilian Lucas 51

3. Salma Abdul 62

4. Paulina David 63

Jumla ya kura zilizopigwa ni 83

Wagombea nafasi za ujumbe Bodi ya Wakurugenzi UTPCW anaume  walioshinda ni

1. Mussa Yusuf 51

2. Cloud Gwandu 61

3. Frank Leonard 64

4. Abdallah Mfaume 69

Kura zilizopigwa ni 83

 

Kundi la wataalam alikuwa mgombea mmoja

Eliazer Mafuru kapata kura zote 83 za ndiyo

 

Kura za Makamu wa Rais UTPC

Wagombea ni

1. Lulu George 18

2. Pendo Mwakyembe 65

Kura halali ni 83

 

Kura za Rais wa UTPC 

1. Deo Nsokolo 72

2. Edwin Soko 11

Kura halali 83

 

Post a Comment

0 Comments