RAIS WA UTPC AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KAGERA KUJIENDELEZA KIELIMU

Na Mwandishi Wetu, Kagera

RAIS wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo, amewataka waandishi wa habari mkoani Kagera kutumia muda huu wa miaka mitano uliotolewa na Serikali kusoma ili kukidhi vigezo vinavyotakiwa na sheria ya huduma kwa vyombo vya habari ya 2016.

Rais Nsokolo alizungumza hayo alipotembelea klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Kagera kwa lengo la kuzungumza na wanahabari juu ya mwelekeo mpya wa UTPC na press club nchini. 

Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo akiwa na viongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kagera (KPC) baada ya kutembelea ofisi hiyo.


Alisema Serikali imeridhia watakaokuwa masomoni baada ya tarehe ya mwisho December 31,2021 kuendelea na kazi wakati wakimalizia masomo yao.

Kwa upande wao waandishi wa habari Mkoa wa Kagera walimshukuru Rais wa UTPC kwa kuwatembelea ikiwa ndio klabu ya kwanza tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo November 17 mjini morogoro.

Nae Katibu wa Kagera Press Club Livinus Feluz alisema wanaamini masuala mengi ambayo yanaikabili tasnia yatapatiwa ufumbuzi katika kipindi hiki na kuahidi kuongeza ushirikiano kwa waandishi wa Kagera.

Post a Comment

0 Comments