Mkuu wa wilaya ya Kibondo bw. Luis Bura (picha na James Jovin ) |
KIBONDO
Mahusiano ya
kibiashara kati ya Tanzania na Burundi yanaendelea kuimalishwa ambapo soko la
kimataifa lililojengwa katika kijiji cha Mkalazi wilayani Kibondo litaanza kutumika
mwishoni mwa mwezi huu likihusisha wafanyabiashara wa nchi za Burundi na
Tanzania
Hayo
yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bw.
Deocres Rutema wakati wa ziara ya pamoja na viongozi wa mkoa wa Ruyigi nchini
Burundi katika eneo ambalo limejengwa soko hilo
Bw. Rutema
amesema kuwa soko hilo litasaidia kukuza
uchumi wa nchi zote mbili lakini pia litasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza
mahusiano mema na kuimalisha ulinzi na usalama kwa kiasi kikubwa
Kwa upande
wake mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya Kibondo bw. Plan Nzuguru amesema
kuwa mahusiano kati ya Tanzania na Burundi yataleta mabadiliko chanya katika
sekta ya uchumi
Aidha mkuu wa mkoa wa Ruyigi nchini Burundi bi. Tabu
Emeransiene amepongeza hatua kubwa iliyofanywa kwa upande wa Tanzania na kwamba
atapeleka ujumbe kwa viongozi wake ili waweze kuanza ujenzi kwa upande wa
Burundi kwa kuwa miradi hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa pande
zote mbili.
Mkuu wa
wilaya ya Kibondo bw. Luis Bura ameshukuru kwa ugeni huo kutoka nchi jirani ya
Burundi na kwamba mahusiano mazuri yamekuwa yakisaidia hata kutatua changamoto
mbali mbali zikiwemo za ulinzi na usalama
0 Comments