Na Mwajabu Kigaza, Kigoma
Wajasiliamali mkoa wa
Kigoma wametakiwa kutumia taasisi za kifedha ili waweze kupata taarifa
mbalimbali zitakazowawezesha kuendeleza biashara zao na kusaidia kuinua uchumi
wa kipato chao.
Kauli hiyo ilitolewa
na meneja kanda ya magharibi Said Pamui kutoka banki ya CRDB wakati wa
semina elekezi ya mpango maalumu kwa wanawake wajasiliamali mpango ambao
utachochea maendeleo yao kwa kutumia fusra za kiuchumi zilizopo mkoani Kigoma.
Viongozi wa Bank ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na wajasilimali wa wilaya za Buhigwe na Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma |
“Hii ni dhana ambayo
itachangia kwa kiasi fulani kuunga mkono juhudi za serikali kuwaletea maendeleo
wananchi hususani wanawake, banki ya CRDB inaamini kwamba kumjuza na kumuelekeza
mwanamke katika fani mbalimbali za ujasiliamali itakuwa imefanikiwa
kuliendeleza Taifa kwa kiwango kikubwa kiuchumi”
Mkuu wa kitengo cha
uwezeshaji wanawake kiuchumi CRDB Rachel Senni amesema lengo ni kumuinua
mwanamke kiuchumi kwa kumpatia elimu ya kupata mikopo, kutunza akiba pamoja na
kufahamu namna ya kutunza kumbukumbu ambapo akaunti ya malkia imeelezwa kuwa
suluhisho la changamoto kwa wajasiliamali wanawake.
Meneja wa bank ya CRDB kanda ya magharibi Said Pamui, akizungumza wakati wa semina ya wajasiliamali wa wilaya za Buhigwe na Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma. |
“Malkia ni akaunti ya malengo ambapo inatumika kuweka fedha kwa
kipindi cha mwaka mzima na unakuwa na malengo ambapo kila siku katika hela ya
faida unatoa 1700 mpaka mwezi unaisha unakuwa na kiasi cha shilingi elfu
51,000/= ambapo kwa mwaka unakuwa na hela ya kutosha lakini pia unaweza
kuitumia kuchukulia mkopo banki” alisema.
Semina hiyo ambayo iliwakutanisha
wajasiliamali wanawake kwa nyakati tofauti katika wilaya ya Buhigwe pamoja
na Manispaa ya Kigoma Ujiji imekuwa na manufaa makubwa ambapo baadhi ya
wajasiliamali walieleza jinsi ambavyo mpango huo utakuwa na msaada kwao ikiwemo
kuepukana na changamoto ya ukosefu wa mitaji, utunzani wa kumbukumbu na
utafutaji wa masoko.
Mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wanawake kiuchumi CRDB Rachel Senni akitoa semina kwa wajasiliamali wilaya za Buhigwe na Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma. |
0 Comments