KIJANA ALIYEFARIKI MIAKA 20 ILIYOPITA AONEKANA MKOANI KIGOMA

Kijana Stewart Edward ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Muhunga Wilayani Kasulu mkoani Kigoma aliyefariki miaka 20 iliyopita na kuonekana tena.


Na Isaac Aron Isaac, Kigoma

Kijana anayefahamika kwa jina la Stewart Edward mkazi wa Kijiji cha Muhunga Wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambaye alifariki Zaidi ya miaka 20 iliyopita amepatikana akiwa hai wilayani humo na kuungana tena na familia yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya wanafamilia kijana akiwemo kaka yake Elia Nikolaus alisema mdogo wake alifariki akiwa na umri wa Takribani miaka nane kwa ugonjwa unaodaiwa kuwa ni Kipindupindu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu ambapo alizikwa na Tangu kipindi hicho hakuwahi kuonekana sehemu yoyote.  

“Tulistaajabu sana kupata taarifa kuwa ndugu yetu ameonekana akiwa hai na tulipoenda kumuona tulikuta kweli ni yeye japo hawei kuongea vizuri ila ni kabisa ndio mana tumekusanyika kufanya sherehe kwakuwa Mungu amemrudisha ndugu yetu” alisema Nikolaus. 


   

Mama mzazi wa kijana huyo Bi Jenita Ruhunzuye alisema licha ya kijana wake kupoteza maisha akiwa na umri mdogo bado aliweza kumtambua baada ya kukutana nae lakini pia kijana mwenyewe inaelezwa kupitia ishara alionyesha kumtambua mama yake jambo lililomtoa machozi ya furaha mama huyo.

“kwa kuwa ni mwanangu niliyemzaa nilipomuangalia tu niligundua ni motto wangu licha ya kuwa umepita muda mrefu na nilipomuita nae alionyesha kunitambua mana alijaribu kuita mama” alisema Bi Jenita.

Tukio hili linahusishwa moja kwa moja na Imani za kishirikina kutokana na mazingira lakini pia ishara alizokuwa akionyesha kijana huyo kuelezea sehemu aliyokuwepo kwani haweza kuongea ingawa alikufa akiwa na uwezo mzuri wa kuzungumza, majirani katika kijiji cha Bugaga wanaelezwa kustaajabishwa na tukio hili.

Hata hivyo Mwaka 2018 tukio kama hili la mtu kufariki kuzikwa na kuonekana tena lilitokea katika kijiji cha Nyumbigwa wilayani Kasulu Mkoani hapa ambapo pia mazingira yake yanahusishwa na Imani za kishirikina kutumika kupoteza watu na kuonekana tena baada ya muda mrefu kupita.

MWISHO

 

 

 

Post a Comment

0 Comments