WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WATAKIWA KUREKEBOSHA KASORO ZA WATENDANI WA SERIKALI

Mkuu wa mkoa wa Kigoma kamishna wa jeshi la polisi Thobias Andengenye amewataka waandishi wa habari mkoani humo, kutumia utaalam wao kurekebisha kasoro ambazo zinasababishwa na watendaji wa Serikali pamoja na wadau wengine ikiwemo taasisi za serikali na binafsi.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Jeshi la polisi Tobias Andengenye mwenye shati nyeupe akiwa na viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Kigoma (KGPC)


Kamishna wa polisi Andengenye amesema wakati akizungumza na Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC Deogratius Nsokolo kuwa, serikali ya mkoa inawategemea waandishi wa habari kuibua masuala mbalimbali ambayo hayatekelezwi kikamilifu. 


Alisema ni wajibu wa waandishi kuandika bila woga wala upendeleo kwa serikali au mdau yeyote, ili mradi kuwe na ulinganifu wa habari .

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa Jeshi la polisi Tobias Andengenye mwenye shati nyeupe akiwa na Mwenyekiti wa  klabu ya waandishi wa habari mkoani Kigoma (KGPC) Deogratius Nsokolo.

"Ili tumsaidie mwananchi  na Taifa letu ni lazima kila mmoja atimize wajibu wake, na nyie waandishi timizeni wajibu wenu serikali mkoani Kigoma itawapa ushirikiano kwa mujibu wa Sheria" alisema

Kwa upande wake Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma Deogratius Nsokolo alisema pamoja na kuhitaji ushirikiano kutoka kwa maafisa wa Serikali na hasa katika kujibu waandishi wanapowahitaji watatimiza wajibu wao kwa kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu na maadili ya uandishi wa habari .


"Mimi siwezi kufika maeneo yote na Wala siwezi kukutana na wananchi wote wa mkoa wa Kigoma na kutatua kero zao, hivyo nawategemea ninyi kujua nini kinaendelea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa, na kila afisa anapaswa kujua ninyi ni msaada kwa wananchi na sio adui" alisisitiza Andengenye

Post a Comment

0 Comments