Gari aina ya Greda likiendelea kuhamisha makaburi eneo la ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji kwaajili ya kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege mkoani Kigoma.
Na Isaac Aron Isaac, Kigoma
Wananchi wa eneo la
Ujiji, Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma ambao wamebomolewa makaburi yao
wameeleza kutoridhishwa na utaratibu unaotumiwa na serikali katika ulipaji wa
fidia ya makaburi hayo kwaajili ya upanuzi wa uwanja wa Ndege wa
mkoa huo.
Wakizungumza na Blog hii baadhi ya wananchi ambao makaburi yao yamevunjwa kwaajili ya kupisha upanuzi wa uwanja walisema utaratibu wa kila mtu kusimama juu ya kaburi ili kulipwa fidia haujatenda haki kulinga na mazingira ya eneo hilo.
Baadhi ya wananchi wa eneo la Ujiji, Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wakiwa wamesimama kwenye makaburi kwaajili kulipwa fidia kabla ya kuhamishwa kwa makaburi hayo.
“Malalamiko yetu ni baada
ya kupewa idadi ndogo ya makaburi kinyume na hali halisi, cha ajabu wengine
hawajalipwa kabisa licha ya kuwa wana makaburi halafu watu wengine hawako
kwenye utaratibu lakini walilipwa” walisema.
Aidha baadhi ya
wananchi walikubaliana na hatua ya serikali “Kuliko kukosa vyote ni kheri
kupata kidogo kilichopo kwani kukataa zoezi la kubomoa makaburi haliwezi saidia
chochote sisi watupatie hizo pesa lakini na wengine hawana budi kukubaliana na
hali ili wakawahifadhi ndugu zao sehemu nyingine” Walisema.
Ngege ya shirika la Ndege Tanzania ikiwa katika uwanja wa ndege wa Kigoma ambao unatarajiwa kufanyiwa malekebisho ya kupanuliwa.
Hata hivyo Uamuzi wa
serikali ukawa ni kuendelea na zoezi hilo licha ya uwepo wa mgomo
kwa baadhi ya wananchi ambapo Meneja wa Tanroad mkoa wa kigoma
Mhandisi Narsisi Choma amesema zoezi hilo la kubomoa
makaburi linaweza chukua siku mbili kisha taratibu nyingine kufuatwa
ikiwemo kumpata mkandarasi ili ujenzi wa upanuzi uanze mara moja
Upanuzi wa Uwanja wa
Kigoma ni moja kati ya hatua ambayo serikali inachukuwa ikiwa ni sehemu ya
kuboresha usafiri wa anga kwani karibu asilimia 40 ya wasafiri wanaotumia
uwanja huo hutokea nchi jirani soko ambalo serikali
inalenga kuliboresha Zaidi.
0 Comments