Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishina wa jeshi la polisi Tibias Andengenye wa pili kutoka kushoto akiwa na baadhi ya viongozi kutoka nchini Burundi wakati wa kikao cha maazimio ya ujirani mwema. |
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Wananchi wa nchi za Tanaznia na Burundi wametakiwa
kuheshimu makubaliano ya amani na ushirikiano baina ya nchi hizo kama viongozi wa nchi hizo walivyo kubaliana kuwa na ushirikiano na kukomesha matukio ya
ujambazi kwa lengo la kuwa na usalama katika pande zote.
Hayo yalizungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina wa jeshi la polisi Thobias Andengenye katika mkutano wa maazimio ya mkutano wa ujirani mwema kati ya mkoa wa Kigoma na mikoa mitaano ya Burundi ambayo ni Makamba, Rutana Ruyigi, Cankuzo na Rumonge.
“Tangu kuanzishwa kwa ushirikiano baina ya nchini hizi
mbili mwaka 2004 kumekuwa na manufaa ambapo kumekuwa na kasi kubwa ya
kutengeneza mazingira wezeshi ili kuendana na kile ambacho viongozi wa nchi hizi
waliadhimia kuendeleza ushirikiano ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali
zilizopo katika nchi zao” alisema Kamishina Andengenye.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Makamba nchini Burundi Bi Francoise
Ngozirazana alisema wataendelea kushirikiana na Tanzania kwani tangu kuanzishwa
kwa ujirani mwema matukio ya uhalifu yamepungua.
“Kigoma imetusaidia sana kutokana na cnhi ya Burundi kuwa
katika vita kwa miaka mingi, naishukuru sana Tanzania kwa kusimama na
kutusaidia kupambana na majambazi waliokuwa wakitaka kuja kuikosesha amani
Burundi” alisema Ngozirazana.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe waliohudhuria kwenye mkutano
huo akiwemo Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia General Marco Gaguti pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Juma Homela walisema hali ya usalama ni shwari licha ya
kuwepo matukio kadhaa ambayo wamefanikiwa kupambana nayo.
0 Comments