KIBONDO
Halimashauri
ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imeanza mkakati wa kilimo cha korosho ambapo
tayari wakulima wamesaidiwa kuanzisha zaidi ya ekali 1800 mpaka sasa na kupewa
elimu ya zao hilo ili kuanzisha kilimo cha biashara kitakachowakomboa kiuchumi
na taifa kwa ujumla
Hayo yamebainishwa
na mratibu wa zao la korosho katika wilaya ya Kibondo bw. Victor Kabunga wakati
wa semina elekezi kwa maafisa ugani na wakulima wa zao hilo juu ya utambuzi wa magonjwa na wadudu
waharibifu wa zao la korosho
Aidha bw.
Kabunga amesema kuwa halimashauri ya wilaya ya Kibondo ilianza rasmi kilimo cha
korosho mwaka 2019 ambapo imekuwa ikitoa elimu kwa wakulima juu ya zao hilo na
kuwapa mbegu bila malipo ili waweze kulima zao hilo litakalowakwamua kiuchumi
Kwa upande
wao baadhi ya wananchi na wakulima wa wilaya ya Kibondo wameonekana
kuchangamkia fursa hiyo na kuanza kulima zao la korosho hata hivyo wameitaka serikali
kuwawekea mazingira mazuri na kuwahakikishia soko la uhakika
Nae afisa
kilimo kutoka bodi ya korosho Tanzania bw. Mandela Chikawe amewahakikishia
wakulima wa zao hilo katika wilaya ya Kibondo kuwa iwapo watalima kwa tija zao
hilo kufikia mwaka 2014 linaweza kuingiza zaidi ya bilioni 7 hivyo kujikwamua
kiuchumi na serikali kwa ujumla. ENDS
0 Comments