MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO APEWA UJAUZITO


 









KIBONDO

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kumsenga iliyoko wilayani Kibondo  anayekadiliwa kuwa na miaka 15 ametorokea kusikojulikana baada ya kupewa ujauzito na kijana wa rika lake ambaye si mwanafunzi

 

Akizungumza na KGPC Blog afisa mtendaji wa kijiji cha Kukinama kata ya Kumsenga bw. Mpaji Juma amesema kuwa mwanafunzi huyo wa darasa la tano pamoja na kijana aliyempa mimba wametoroka wote kwa pamoja ikiwa ni masaa machache baada ya kupewa wito wa kufika ofisi za kijiji wao pamoja na wazazi wao

 

Aidha amesema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa tayari ameacha shule zaidi ya miezi miwili iliyopita na inaonekana wazazi wa pande zote mbili huenda wanahusika na walikuwa katika mpango wa kuwaozesha vijana wao kwa kuwa licha ya kumuona kijana wao akiwa na mimba lakini hawakutoa taarifa popote

 

Baada ya watoto hao kutoroka wazazi wa pande zote mbili wamekamatwa na kufikishwa kituo kidogo cha polisi kumsenga ili waweze kuwajibishwa kwa kuwa inaonekana wamehusika kwa namna moja ama nyingine katika tukio hilo lililopelekea mwanafunzi huyo wa darasa la tano kupoteza ndoto zake. ENDS

Post a Comment

0 Comments