Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Sekta ya Afya mkoani
Kigoma imeeleza katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018 imefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu
ambacho kilikuwa kikiathiri eneo kubwa la mkoa huo.
Mganga mkuu wa mkoa wa
Kigoma Dkt Saimon Chacha alieleza hayo wakati wa makabidhiano ya vifaa kwaajili
ya wahudumu wa afya kutoka taasisi ya Benjamini Mkapa vilivyo na thamani ya
million 74 kwa lengo la kusaidia kuwakinga watoa huduma na magonjwa mbalimbali
ya mlipuko.
Ni miaka mitatu ya
jitihada kubwa kwa sekta ya afya mkoani Kigoma ambayo iliongeza kasi baada ya
kuingia kwa maambukizi ya Covid 19 ambapo wagonjwa sita pekee walipata
maambukizi hayo, lakini kipindupindu imekuwa kadhia ya muda marefu kwa wakazi
wa mkoa huu.
Jitihada hizo
zinachagizwa na wadau wa maendeleo ambao nao wanaona ipo haja ya kuimarisha
idadi ya watoa huduma za afya ambao kwa mkoa wa Kigoma bado ni ndogo ambapo
taasisi ya Benjamini Mkapa imefanikiwa kuajiri watia huduma 197 katika vituo
vya afya mkoani hapa sambamba na utoaji wa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya
maambukizi katika halmashuri zote nane.
Sehemu ya vifaa vilivyotolewa na taasisi ya Benjamini Mkapa kwaajili ya kwaajili ya wahudumu |
Mchango wa wadau wa
maendeleo katika sekta ya afya kwanza kabisa ukapongezwa na mkuu wa mkoa wa
kigoma Thobias Andengeye kisha kibao kikageukia kwa watumishi wa afya ambao
ndio wako mstari wa mbele kuhakikisha hali ya kiafya mkoani hapa inazidi
kuimarika kuhakikisha wanatumia taaluma yao vyema kulinda mkoa wa Kigoma.
0 Comments