WAFANYABIASHARA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI WAIJIA JUU SERIKALI

 


Na Mwandishi Wetu, Kigoma.

Wafanyabiashara katika Soko la Kigoma Mjini Manispaa ya Kigoma Ujiji, wameuomba uongozi wa Manispaa hiyo, kuujengea ukuta mfereji wa Rubengela unaopita katika soko hilo.

Hiyo ni baada ya baadhi ya biashara kusimama kufuatia vibanda vitano vya biashara kubomoka kutokana na mmomonyoo wa udongo uliosababishwa na mfereji huo unaomwaga maji katika Ziwa Tangayika.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Kigoma Juma Chaurembo, alisema tatizo hilo ni la muda mrefu na tayari wamelitolea taarifa kwa mamlaka husika kabla ya madhara zaidi kutokea lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Baraka Lupoli akijibu malalamiko ya wafanyabiashaara hao alisema, tatizo hilo limefikshwa kwa jopo la wakandarasi kwa ajili ya kulishughulikia na kulipatia ufumbuzi.

 

Post a Comment

0 Comments