WAKUTWA WAKIUZA NYAMA YA MBWA


 











KIBONDO

 

Watu watatu wakazi wa kijiji cha Kigina kata ya Rugongwe wanashikiliwa na serikali ya kijiji hicho kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara haramu ya kuuza nyama za Mbwa kinyume na maadili ya kitanzania

 

Akizungumza na KGPC Blog afisa mtendaji wa kijiji hicho bw. Shedrack Totoye amewataja watuhumiwa hao  kuwa ni Bahati Ngubaguba, Lucas Shija pamoja na Ndikumana Paul wote wakazi wa kijiji cha Kigina

 

Aidh bw. Shedrack amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa hapo jana January 11 katika soko la Kitongoji cha Malimbi kijiji cha Kigina ambapo wamekuwa wakichanganya nyama ya mbwa pamoja na mbuzi au Nguruwe na kuwauzia wananchi kwa masirahi yao binafsi

 

Mmoja wa watuhumiwa hao bw. Bahati Ngubaguba akizungumza na redio kwizera amekili kujihusisha na biashara hiyo ambapo amesema kuwa amekuwa akiwauzia wananchi wanaopenda nyama hiyo ambapo pia yeye mwenyewe amekuwa akiitumia kama kitoweo, Tayari watuhumiwa wote wamefikishwa kituo kidogo cha polisi Rugongwe kwa mahojiano zaidi. ENDS


Post a Comment

0 Comments