KIBONDO
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la muhambwe wilayani
Kibondo mkoani Kigoma amezikwa leo kijijini kwao Kumwambu kufuatia ajali
aliyoipata February 10 eneo la nane nane jijini Dodoma na kufariki dunia February
13 wakati akipatiwa matibabu.
Mazishi hayo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali
wa serikali akiwemo waziri mkuu wa Tanzania Majaliwa kasimu, Naibu sipika Tulia
akisoni, waziri wa elimu profesa Joyce Ndalichako aliyewakilisha wabunge wa
mkoa wa Kigoma
Waziri mkuu kasimu Majaliwa akitoa salamu za rambi
rambi amesema kuwa marehemu Atashasta Nditiye wakati wa uhai wake alifanya kazi
kwa uadilifu mkubwa na kuwatumikia
wananchi kwa upendo hivyo pengo lake ni kubwa katika jamii na familia yake kwa
ujumla
Kwa upande wake waziri wa Elimu profesa Joyce
Ndarichako pamoja na naibu spika Tulia Akisoni wakitoa salamu zao za rambi
rambi wamesema kuwa marehemu Atashasta Nditiye ni moja kati ya wabunge ambao
walijitolea sana kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya taifa na jamii kwa
ujumla.
Baadhi ya wananchi wanaoishi katika jimbo la
Muhambwe wamepokea kifo cha mbunge wao kwa masikitiko makubwa kwa kuwa alikuwa
mbunge mwenye mipango mingi ya maendeleo
Misa ya mazishi na kumuaga marehemu imefanyika
katika kanisa Anglikana la mtakatifu Hilario kanisa kuu la dayosisi ya Kibondo
misa ikiongozwa na baba askofu Sospiter Temeo Ndenza
Marehemu Nditiye amefariki kwa ajali ya gari akiwa
na umri wa miaka 52 ambapo ameacha mke na watoto watatu katika kipindi hiki
ambapo alikuwa amechaguliwa kulitumikia jimbo la muhambwe kwa awamu ya pili,
bwana alitoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.
0 Comments