Na Adela Madyane, Kigoma
Licha ya ukuaji wa
tasnia ya habari nchini wanawake bado wanakabiliwa na Changamoto nyingi kwani
nafasi nyingi za uongozi zinasimamiwa na wanaume na si wanawake.
Changamoto kubwa ambayo wanawake wameendelea kukabiliana nayo ni umiliki
wa vyombo vya habari kwani vingi humilikiwa na wanaume hivyo huwapa nguvu
wanaume wenzao na wanawake kubaki kama waandishi wa habari na si kama wahariri
au mameneja. Japo wapo wanawake wahariri lakini bado kuna namna ya kufanya
kwaajili ya kuongeza idadi yao
Na hii ndio sababu hasa inakuwa ngumu kushinikiza na kujumuisha masuala
ya usawa wa kijinsia kwasababu wanawake wengi hawapo karibu na chombo Cha
kufanya maamuzi
Tunaposherehekea siku ya wanawake duniani yenye kichwa "wanawake
katika uongozi katika ulimwengu wa COVID-19 kuna haja wanawake wakavaa vazi
katika nafasi za juu za uongozi , wanawake hawapaswi kuogopa kutafuta fursa za
ukuaji katika taaluma yao
Katika kipindi hiki Cha COVID-19, wanawake na wanaume hodari katika tasnia ya
habari wamekuwa wakiendelea kufanya kazi vizuri katika kutoa habari muhimu kwa
umma jambo ambalo linapaswa kuhimizwa na kupongezwa vilivyo.
Hivyo kutokana na juhudi hizo itapendeza kwamba sera za vyombo vya habari
kuendelea kuhimiza na kulazimisha wamiliki wa vyombo vya habari
kuteua asilimia fulani ya wanawake katika nafasi za juu ya kufanya maamuzi,
itapendeza ikiwa 50/50 au 50/60 kutokana na wanawake kuwa wengi kiidadi
Na kwa wanawake ambao tayari ni wahariri na wanashika nyadhifa mbalimbali
katika vyombo vya habari wanapaswa kuacha kuharibu mitazamo ambayo inaharibu
taswira ya mwanamke lakini badala yake wawawezeshe wanawake wenzao kuchukua
nyadhifa pia Ili kuinua taaluma yao, familia zao na taifa kwa
ujumla.
0 Comments