MCHAKATO WA UBUNGE JIMBO LA MUHAMBWE

 Na Deogratius Nsokolo, Kibondo

Wanachama 25 wa Chama cha Mapinduzi CCM, wamechukua fomu kuwania ubunge katika Jimbo la Muhambwe Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo na naibu waziri wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi wa zamani Mh.Atashasta Nditiye kufariki dunia February 12 mwaka huu.



miongoni mwa waliochukua fomu ni mbunge wa zamani wa Jimbo hilo na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Kijiko, mfanyabiashara Jamal Tamim na Daktari Florence Samizi.





wengine wanaogombea uchaguzi huo ni mhandisi Dickson Bidebeli, Dr. Donasiana Stephano, Shukuru Gwamagobe, Flbert Nisuzi, Nduhilibusa Mapigano, Dr. Joseph Tutuba, Juhudi Ngarama, Zabron Wailalo, Nyinisaeli Gwamagobe na mwandishi wa habari Prosper Kwigize.





Katibu huyo wa ccm wilaya amewataja wengine kuwa ni david Ntezidyo, Hassan Mgutta, Dr. Chrispine Shami, Fredrick Rulagilije, Regina Kayabu, Dyagombwa Ntimba, Amina Kanyogoto, Dr. Arkado Barakabise, Philipa Mturano, Richard Makera, Adrian Sabudema na Baraka Budogo.


Zoezi ndani ya CCM lilianza machi 24,2021 na kukamilika marchi 25, ambapo wote waliochukua walifanikiwa kuzirejesha.




Kaimu Katibu wa chama cha Mapinduzi Wilaya kibondo Tausi Feruzi alisema baada ya kukamilika kwa zoezi la uchukuaji fomu na kuzirudisha kukamilika, upigaji kura za maoji utafanyika leo (jumamosi mach 27 ) kwa ajili ya kumpata Mtu atakaye peperusha Bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mei pili mwaka huu.


Amesema Wagombea wote wamepewa maelekezo ya kufanya ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya  rushwa na atakayebainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.




Tume ya Taifa ya uchaguzi kupitia kwa Mkurugenzi mkuu wa uchaguzi Dkt. Wilson Mhera imetoa ratiba ya uchaguzi ikionyesha kuwa wagombea kupitia vyama mbalimbali vya siasa watachukua fomu kwa msimamizi wa uchaguzi tarehe 28 machi hadi tarehe 3 April ambayo pia itakuwa ndio siku ya uteuzi wa wagombea, Kampeni zitaanza April 4 hadi mei mosi na uchaguzi utafanyika mei 2, 2021.


Uchaguzi katika jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama cha mapinduzi mhandsi Atashasta Nditiye aliyefariki February 12 kwa ajali mjini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments