MKUU WA WILAYA KASULU AIOMBA SERIKALI KUPITISHA ADHABU KWA WANAFUNZI WANAOPATA MIMBA

 


Na Mwandishi Wetu Kasulu, Kigoma

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Kanal Saimon Anange ameiomba serikali kupitisha sheria ya adhabu kwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni ili kusaidia kupambana na changamoto hiyo.

Kanal Anange amesema hayo katika hafla iliyowakutanisha wadau wa elimu, waalimu na wanafunzi ambapo amesema sheria iliyopo kwa sasa ya kifungo cha miaka 30 jela inapaswa kutumika kwa wote wawili pale wanapokutwa na hatia.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari hapa Mkoani Kigoma wamesema endepo sheria hiyo ikifanyiwa  marekebisho itakuwa na tija katika kupambana na mimba mashuleni.

 

Post a Comment

0 Comments