WANANCHI KIGOMA WAMPONGEZA DKT MPANGO KUTEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS



Kufutia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassan kumteua aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais kisha bunge kumthibitisha, Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wametoa maoni yao juu ya uteuzi huo.

 

Wanannchi hao wamesema wanaimani kutokana na rekodi yake ya kazi katika idara, sekta na wizara ya fedha kuwa atakuwa na nafasi ya kusaidia kukua kwa uchumi na kusimamia miradi ya maendeleo katika Taifa.

 

Doroth Timos na Stansilaus Bujiji ni miongoni mwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma wamesema uteuzi huo utakamilisha mipango ya aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati Magufuli kwa kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo na kuchochea uchumi kwa wananchi na Taifa.

Post a Comment

0 Comments